Rais Uhuru Kenyatta Kushughulikia Marekebisho ya Mfumo wa Mtihani wa Wanafunzi Walemavu

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kushughulikia ombi la wanafunzi walemavu la kufanyia marekebisho mfumo wa mitihani ulioko sasa. Wanafunzi hao wanataka mitihani kuwasilishwa kwao kwa njia watakazo-mudu.

Wanafunzi hao ambao ni sehemu ya kundi la vijana walioshiriki kwenye mpango wa Rais wa utoaji tuzo; kwa kushirikiana na mradi wa kimataifa wa utoaji tuzo unaofahamika kama (Seeing is Believing), yaani:- a�?Kuona ndio Kuaminia�?, unaodhaminiwa na Duke wa Edinburgh; walisema ijapo wana akili sawa na wanafunzi wengine, wao huanguka kutokana na hali yao ya ulemavu.

Kwa sasa wanaomba kupewa nafasi kupitia taratibu nyingine ambazo zitawawezesha kushindana na wenzao katika viwango sawa. Rais Kenyatta alisema atachunguza ombi hilo na kutoa jawabu hivi karibuni. Katibu wa wizara ya elimu, Dr. Belio Kipsanga�� na waziri wa mazingira Judy Wakhungu pia walihudhuria hafla hiyo