Mfumo Duni Wachangia Ufisadi Kwenye Kaunti-Agness Adhiambo

Msimamizi wa bajeti, Agnes Odhiambo amesema kukithiri kwa ufisadi katika serikali za kaunti kunachangiwa na mfumoA�duni wa uhasibu katika serikali hizo. Akiongea kwenye kongamano la tano la kila mwaka la tume za kikatiba na afisi huru, Bi Odhiambo alisema mfumo hafifu wa uhasibu katika maeneo ya kaunti unatatiza vita dhidi ya ufisadi. Alimtaka mkaguzi mkuu wa hesabu,A�Edward Ouko kubainishaA�iwapo wakenya wanapata thamani ya pesa zao au la. Ouko alielezea wasi wasi kuhusu kushindwa kwa asasi za upelelezi hapa nchini kuhakikisha kesi zaA�ufisadi zinashughulikiwa ipasavyo. Hayo yamejiri huku madai zaidi ya ufujaji pesa yakiibuka katika maeneo ya kaunti hususan kaunti ya Kilifi ambapo serikali hiyo imekiri kutoweka kwa shilingi milioni-51 kupitia kandarasi za udanganyifu.