Mfanyabiashara Wa Nairobi Jacob Juma auawa

Mfanyabiashara kinzani wa Nairobi Jacob Juma ameuawa.Juma aliuawa kwa kupigwa risasi A�jana usiku akiwa ndani ya gari lake A�kwenye barabara ya A�Ngong karibu na shule ya A�Lenana,hapa Nairobi.Afisa mkuu wa idara ya upelelezi hapa Nairobi Ireri Kamwende alisema mfanyabiashara huyo alikumbana na mauti mwendo wa A�saa tatu na nusu usiku na majambazi waliokuwa kwenye pikipiki alipokuwa akitoka baa yake.Ilisemekana Juma A�ambaye amekuwa msitari wa mbele kwa kufichua A�kashfa alipigwa risasi mara kumi.Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 42 ameibua mijadala mikali A�kuhusu maswala ya kisiasa hapa nchini.Marehemu atakumbukwa kutokana na madai kuwa leseni yake ya utafiti nas uchimbuaji wa madini ilifutiliwa mbali alipokataa kutoa hongo kwa aliyekuwa waziri wa A�madini Najib Balala.Hata hivyo Balla alipuuzilia mbali madai hayo,akiyataja kuwa za kutaka kumharibia sifa.Aidha mfanyabiashara huyo alikataa kumwomba msamaha jaji wa mahakama ya juu nchini Njoki Ndunga��u kwa madai kuwa jaji huyo alipokea pesa A�pamoja na jaji Philip Tunoi anayekabiliwa na kesi ya utoaji hongo.Ndunga��u alikanusha madai hayo.

A�