Mexico,Marekani zakubaliana kufanyia mkataba wa biashara huru

Serikali za Marekani na Mexico zimekubaliana kufanyia marekebisho mkataba wa biashara huru kati ya mataifa ya Marekani ya Kaskazini.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye awali alikashifu mkataba ulioko kwa sasa amesema makubaliano hayo yatakuwa ya manufaa makubwa. Canada ambayo ni mwanachama wa mkataba huo bado haijakubaliana na marekebisho yaliyofanyiwa mkataba huo.

Trump alitishia kujiondoa kutoka mkataba huo akidai umesababisha kupungua kwa ajira kwenye viwanda vya utengenezaji bidhaa hususan utengenezaji magari.