Messi afunga bao lake la 500 na kuisaidia barcelona kuibuka washindi dhidi ya Real Madrid

Lionel Messi alifunga bao lake la 500 katika timu ya Barcelona na kuisaidia timu hiyo kuchupa uongozini mwa ligi kuu nchini Uhispania baada ya kuilaza Real Madrid mabao 3-2 katika mechi ya kusisimua yaA� El-classico iliyochezwa jana usiku. Barcelona sasa ina alama sawa na Real Madrid ambayo haijacheza mechi moja. KwinginekoManchester United iliendeleza jitihada zake za kumaliza miongoni mwa timu nne bora ligini baada ya kuilaza Burnley mabao 2-0 katika mchuano wa ligi kuu uingereza. Wayne Rooney alimuandalia pasi Anthony Martial aaliyefunga bao la kwanza kabla ya nahodha huyo wa UingerezaA� kuongeza la pili, likiwa ni bao lake la kwanza tangu mwezi January mwaka huu.Kufuatia ushindi huo United inasalia katika nafasi ya tano alama sawa na wakinzani Manchester City.Timu hizo mbili Manchester United na Manchester City zitamenyanaA� alhamisi hii ugani Etihad.