Meddie Kagere atajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka

Mshambulizi wa Gor Mahia Meddie Kagere ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wanahabari wa michezo humu nchini SJAK. Kagere alituzwa wakati wa hafla iliyoandaliwa jana usiku jijini Nairobi. Kagere alifunga mabao 13 katika msimu wa mwaka huu na kuisaidia Gor Mahia kutwaa taji ya ligi ya Sportpesa na kumpiku mwenzake George Blackberry Odhiambo katika tuzo hizo. Kagere pia alimshinda kiungo wa Kariobangi Sharks Masud Juma. Mlindalango wa Kariobangi Sharks Jeff Oyemba alitwaa tuzo ya mlindalango bora wa mwaka huku akiwashinda Patrick Matasi na David Juma. Tuzo ya kocha bora iilitwaliwa na kocha wa Sofapaka Sam Ssimbwa huku George Blackberry Odhiambo wa Gor Mahia akitajwa kiungo bora wa mwaka. Mchezaji mwingine wa Gor Mahia Musa Mohhamed alitajwa mlinzi bora wa mwaka na kumpiku mwenzake Godfrey Walusimbi na Jockins Atudo wa Posta Rangers. Kiungo wa Zoo FC Nicholas Kipkurui alishinda tuzo ya mchezaji chipukizi wa mwaka huku kiungo wa Kariobangi Sharks Masoud Juma akitwaa tuzo ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao 17 msimuni.