Mechi ya ligi kuu baina ya AFC Leopards na Wazito yaahairishwa

Mechi ya ligi kuu ya soka humu nchini baina ya AFC Leopards na Wazito imeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Leopards, mabingwa mara 13 wa ligi kuu, hawakushiriki ligini mwishoni mwa juma kwasababu walikuwa wakichuana na Fosa Juniors ya Madagascar, katika mechi ya kuwania kombe la mashirikisho. Mechi hiyo baina ya Leopards na Wazito iliratibiwa kuchezwa Alhamisi hii lakini sasa imeahirishwa. Wakati uo huo, droo ya mashindano ya timu nane bora ya KPL, imeahirishwa hadi mwezi ujao.Kimataifa, Kick It Out, shirikisho linalopambana na ubaguzi wa rangi katika soka, limeeleza kutoridhishwa kwake na kadi ya njano aliyooneshwa Mario Ballotelli kwa kulalamikia matusi ya ubaguzi wakati wa mchuano wa ligi ya Ufaransa mwishoni mwa juma. Ballotelli, aliyezichezea timu zaA�Manchester City, Liverpool na Italia awali, alioneshwa kadi ya njano na refa Nicolas Rainville katika kipindi cha pili cha mchuano baina ya Nice na Dijon, kwa kulalamika kuhusu matusi ya ubaguzi wa rangi ya mashabiki wa Dijon.