Mdahalo wa wagombeaji urais hatimaye waandaliwa

Mdahalo wa wagombeaji urais uliosubiriwa kwa hamu hatimaye ulianza jana mwendo wa saa kumi na moja unusu jioni katika chuo kikuu cha kanisa katoliki kilichoko Karen, jijini Nairobi. Wagombeaji watatu dakta Ekuru Aukot wa Third way Alliance, Profesa Michael Wainaina na DaktaJapheth Kaluyu ambao ni wagombeaji huru walijitokeza kwa awamu ya kwanza ya mdahalo huo. Watatu hao walitaja ukabila, ufisadi na ukosefu wa ajira kuwa changamoto kuu zinazokumba nchi hii. Waliwarai Wakenya kufungua ukurasa mpya kwa kuwachagua viongozi waadilifu A�watakaojali maslahi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi ujao. Walidai kuwa chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta A�au muungano wa NASA haiwezi kuaminika kuleta mabadiliko yanayohitajika humu nchini. Awamu ya pili ya mdahalo huo ilitarajiwa kuwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mgombeaji wa muungano wa NASA Raila Odinga. Wagombeaji wengine Cyrus Jirongo, Joseph Nyagah na Abduba Dida pia walialikwa lakini hawakushiriki.