Mchezaji Wa Gor Victor Abondo Ajaribiwa Na Klabu Ya Ajax Cape Town, Afrika Kusini

Kiungo wa timu ya Gor Mahia Victor Ali Abondo, yuko nchini Afrika Kusini anakohudhuria majaribio kilabuni Ajax Cape Town. Abondo aliyejiunga na Gor Mahia mwaka 2014, A�amemfurahisha kocha mkuu wa Ajax, Rodger de Sa na atafanya mazoezi na timu hiyo katika majuma kadhaa yajayo kutathmini uwezo wake. Akiongea na Supersport.com A�kutoka Afrika Kusini, Abondo alisema amefuraishwa na mazoezi na anatarajia matokeo mema.

Aidha, Abondo alitekeleza jukumu muhimu msimu uliopita kwenye timu ya Gor Mahia ambapo alifunga mabao matatu katika mechi za ligi ya kilabu bingwa barani Afrika na mabao 11 katika ligi kuu ya soka humu nchini na kusaidia KOa��galo kuhifadhi taji yake bila kushindwa.