Mbunge Wambui akanusha kuhusika na ulaguzi wa mihadarati

Mbunge wa Othaya, Mary Wambui amekanusha kuhusika na ulanguzi wa mihadarati kufuatia habari zilizochapishwa kwenye gazeti moja humu nchini zikimtaja kuwa miongoni mwa wanasiasa wakuu wanaohusika na biashara hiyo haramu. Wambui alijitenga na habari hizo, akisema yeye ni mcha Mungu na kwamba hahusiki na mihadarati. Mbunge huyo alisema hayo alipozuru eneo bunge lake kuwahimiza wakazi kusajiliwa kuwa wapigaji kura katika shughuli inayoendelea. Mbunge huyo alisema eneo hilo limeandikisha idadi ndogo ya watu wanaojisajili katika kaunti hiyo, akisema anatumai watu zaidi watajitokeza ili kuongeza idadi hiyo ingawa huenda lisiafikie lengo lililokusudiwa. Kulingana na tume ya IEBC, eneo hilo kufikia siku ya jumatatu lilikuwa limesajili takriban wapigaji kura wapya 5,500 ikilinganishwa na idadi ya watu elfu 19 inayokusudiwa huku A�shughuli hiyo ikikaribia kumalizika. A�