Mbunge wa Tiaty ataka kamati ya bunge kujadilia marekebisho ya bajeti

Mbunge wa TiatyA� William Kassait Kamket anataka kamati ya bunge la taifa kuhusu bajeti kuruhusu kujadiliwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba unaolenga kushinikiza kubuniwa kwa wadhifa wa waziri mkuu na pia kufanyia mageuzi mfumo wa maongozi. Kamket anapendekeza kubuniwa tena kwa wadhifa wa waziri mkuu ambaye atachaguliwa na wabunge na kupewa mamlaka . Hivyo basi raisA� hatakuwa na mamlaka na atakuwa ishara ya umoja wa kitaifa. Kamket anapendekeza kuwa rais , wabunge na magavana wachaguliwe na wakenya huku maseneta wakichaguliwa na wanachama wa mabunge ya kaunti. Kulingana na mswada huo wadhifa wa mwakilishi wa wanawake unafaa kufutiliwa mbali kwa sababu maeneo bunge yanawakilishwa na maseneta na magavana.

Hata hivyo wanachama wa kamati ya bajeti wamehoji jinsi mswada huo utakavyoimarisha ujumuishaji katika maongozi wakati chama kikubwa zaidi ndicho kitakachoamua uchaguzi wa waziri mkuu. Iwapo mswada huo utaidhinishwa na bunge , utalazimika kupigiwa kura ya maamuzi kwa sababu unabadilisha sera za maongozi jinsi ilivyoratibishwa kwenye katiba.