Mbunge wa Nyeri mjini awasilisha rufaa dhidi ya Jaji mkuu David Maranga

Mbunge wa Nyeri mjini, Ngunjiri Wambugu, amewasilisha rufaa yake kwa tume ya idara ya mahakama -JSC kutaka jaji mkuu David Maraga aondolewe ofisini kufuatia kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais wa tarehe 8 Augosti. Katika rufaa hiyo yenye kurasa 14, Wambugu anadai kwamba wakati wa kusikizwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais, jaji mkuu alishawishiwa na matamshi ya kisiasaA� kutoka kwa muungano wa upinzani a�� NASA, kabla ya muungano huo kuwasilisha kesi yake mahakamani. Anadai kwamba Justice Maraga hakusomaA� ushahidi wote uliowasilishwa mbele yake wakati wa kusikiza kesi hiyo. Wambugu amefananisha kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais wa tarehe 8 Augosti naA� mapinduzi ya kisheria, ndiposa anataka malengo ya Maraga kuchunguzwa. Lakini katika tukio jingine, wakili mmoja wa Jijini Nairobi, Dunstan Omari amesema sheria haitambui kitu chochote kama mapinduzi ya ki-sheria, huku akitaja taratibu za kuondolewa ofisini kwa jaji mkuu kuambatana na kifungu cha 168 cha katiba ya nchi hii. Alisema kwamba kuondolewa ofisini kwa jaji mkuu sio jambo rahisi, akiongeza kwamba juhudi za wale wanaojihusisha na jambo kama hilo hazitawafikisha popote. Mahakama ya juu ilifutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais ikitaja kasoro na pia ukiukaji sheria katika upeperushaji matokeo na tume ya IEBC.