Mbunge wa Kitui magharibi Francis Nyenze afariki

Mbunge wa Kitui magharibi Francis Nyenze amefariki leo asubuhi alipokuwa akipata matibabu katika Nairobi Hospital.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha wafu cha Lee hapa Nairobi. Francis Nyenze alizaliwa tarehe mbili mwezi june mwaka 1957 huko A�Kabati, Kitui magharibi. Alikuwa kiongozi wa wachache bungeni kabla ya uchaguzi.Mwaka A�2001 alikuwa waziri wa michezo baada ya kuhudumu kama waziri wa mazingira mwaka 1997.Dalili za kuwa na hali duni ya afya zilionekana alipoapishwa kwenye bunge la 13 alipofika bungeni akionekana mdhaifu. .Alikuwa mwanachama wa Wiper lakini alizua hisia wakati yeye pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho David Musila walipounga mkono kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta wakati wa uchaguzi wa tarehe 8 mwezi agosti mwaka huu.Alizua hisia tena wakati alipotangaza kwamba Kalonzo Musyoka nduey atakayepeperusha bendera ya nasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.Ni matamshi yaliokashifiwa vikali na wenzake katika chama cha Wiper.