Mbunge Wa Garissa Aden Duale Alalamikia Ukosefu Wa Maji Garissa

Mbunge wa Garissa mjini Aden Duale amesema serikali ya kitaifa huenda ikatwaa jukumu la usambazaji wa maji kutoka kwa kampuni ya maji  ya  Garissa (GAWASCO) ili kukomesha tatizo la maji linalokumba  mji huo.  Duale amesema uhaba  wa sasa wa maji unazidi na serikali ya kitaifa haitaruhusu  wakazi kuendelea kuteseka. Akiwahutubia  wanahabari  mjini  Garissa  ,Duale  aliye pia kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa alisema serikali ya kaunti hiyo imeshindwa kabisa  kutekeleza wajibu wake wa kuwapa maji wakazi wa mji wa Garissa . Alisema wakazi hao hupoteza muda mwingi kutafuta maji badala ya kujihusisha katika shughuli muhimu za kiuchumi. Alisema pesa zikipatikana sabuni za utoaji maji zitatangazwa . Alisema kampuni ya maji na majitaka ya Garissa na bodi ya maji ya eneo la Kaskazini haziaminiki tena kupatiwa pesa za umma.  Gavana wa kaunti hiyo  Nathif Jama jana alimshtumu Duale akisema anafaa kukoma kuingiza siasa tatizo la uhaba wa maji.