Mbunge Arama afikishwa mahakamani

Mbunge wa Nakuru Mjini Magharibi, Samuel Arama leo alifikishwa kwenye mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi baada ya kukamatwa Ijumaa iliyopita kuhusiana na ununuzi wa kipande cha ardhi kinachozozaniwa. Arama alikanusha mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkuu Douglas Ogoti. Arama anadaiwa kutumia vibaya mamlaka, kupanga njama ya kulaghai, kughushi stakabadhi na kuwadanganya maafisa wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi.

Alishtakiwa pamoja na Kennedy Onkoba ambaye pia alikanusha mashtaka. Arama na mwenzake wamewekwa rumande kusubiri uamuzi kuhusu ombi lao la dhamana hapo kesho. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Noordin Haji, Arama anatuhumiwa kushirikiana na maafisa wa idara ya usajili wa ardhi huko Nakuru kupata stakabadhi za kumiliki kipande hicho cha ardhi