Mbunge Amtetea Kalonzo Dhidi Ya Madai Ya Unyakuzi Wa Ardhi

Mbunge wa Mavoko Patrick Makau, amemtetea kiongozi wa A�chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kutokana na madai kuwa alinyakua ardhi ya ekari 4,000 katika eneo laA� A�Mavoko. Makau amesema kama mbunge wa eneo hilo hana habari A�kuwa Kalonzo anamiliki ardhi katika eneo hilo. Amepuuzilia mbali madai ya gavana wa A�Machakos A�Alfred Mutua na kuyataja kuwa propaganda inayolenga kumharibia sifa Kalonzo. Makau amesema tuzo ya hivi majuzi ambayo Kalonzo alishinda mjini A�New York inadhitibitishia ulimwengu kuwa ana maadili mema na ni kiongozi anayeheshimika ambaye anaweza kuunganisha taifa hili.A� A�Makau alikuwa akiongea katika kijiji cha ilgarooj, eneo-bunge la Kajiado Magharibi kaunti ya Kajiado wakati wa hafla ya maombi iliyoandaliwa ili kuombea amani hapa nchini. Kalonzo ambaye alihudhuria hafla hiyo hakujibu madai hayo lakini aliangazia ufisadi unaoshuhudiwa hapa nchini na kusisitiza haja ya kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya wahusika.