Mazungumzo Kuhusu IEBC Kuendelea Leo

Mazungumzo kuhusu masharti ya kuondoka ofisini kwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka (IEBC) yatarejelewa leo baada ya A�makamishna hao kuomba muda zaidi wa kuratibu ripoti ya mwaka ambayo makataa yake ni leo tarehe 30 septemba. Pia watatumia muda mchache uliosalia kushauriana na kupokea michango ya makamishna wote. Inadaiwa kwamba makamishna hao wamekuwa wakiitisha mshahara wa miezi 13, kiinua mgongo A�na pia mkopo wa kununulia gari. Hapo jana kundi hilo la (IEBC) A�likiongozwa na mwenyekiti wao Isaak Hassan lilipewa muda wa siku moja kujadili swala hilo baada ya mazungumzo baina yao na maafisa wa serikali kugonga mwamba. Mkutano huo uliongozwa na kamati maalum inayoshirikisha waakilishi wa wizara ya fedha, afisi ya mwana-sheria mkuu, wizara ya utumishi wa umma, na pia afisi ya Rais kama mwakilishi wa serikali. Vuta ni kuvute kati ya serikali naA� A�makamishna hao wa (IEBC), inajiri huku wataalamu wakionya kwamba mpango wa kuitisha uchaguzi mkuu tarehe 8 Augosti mwaka 2017 huenda hautawezekana ikizingatiwa sheria mpya kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi ambayo itaanza kutekelezwa katika muda wa juma moja lijalo. Kwa mujibu wa wataalamu hao sheria hiyo inatoa changamoto kadhaa kwa tume ya (IEBC). Changamoto hizo ni pamoja na masharti makali kuhusu ukaguzi wa sajili ya wapiga kura, na utumizi wa teknolojia ambayo itatatizika vibaya na sheria kuhusu ununuzi wa A�bidhaa.