Usalama Waimarishwa Katika Mazishi Ya Mark Too

Maafisa zaidi wa usalama wamepelekwa nyumbani kwake aliyekuwa mbunge maalumu Mark Too, katika shamba la maziwa, kaunti ya Uasin Gishu kabla ya mazishi yake A�hivi leo. Too mwenye umri wa miaka 64 alifariki kutokana na matatizo ya moyo wakati wa mkesha wa mwaka mpya katika hospitali ya St.Luke’s huko Eldoret. Agizo la mahakama la kusimamisha mazishi hayo lililokuwa limetolewa kwa ombi la wakili wa Eldoret Simon Lilan, limeondolewa A�kwa ombi la wakili wa familia Profeesa Tom Ojienda na sasa mazishi yake yataandaliwa leo kama ilivyopangwa. Wakili huyo alikuwa akitaka mazishi ya mwanasiasa huyo yasimamishwe kutoa fursa ya kufanya uchunguzi wa kubainisha kiini cha kifo chake. Mazishi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na wanasiasa. Too alizaliwa katika eneo la Ndebunet, kaunti ya Nandi mwaka A�1952 na alihudumu katika serikali ya rais mstaafu Daniel Arap Moi katika wadhifa wa waziri msaidizi.

Wakati huo huo mwanamke mmoja aliyejaribu kuzuia kuzikwa kwa aliyekuwa mbunge maalum Mark Too alipelekwa hospitalini leo asubuhi baada ya kuzirai katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Fatuma Ramadhan alikuwa akielekea katika hafla ya mazishi ya Too huko Eldoret pamoja na mwanawe na wakili wao Danstan Omari. Omari amesema waliwasili katika uwanja huo wa ndege mwendo wa saa 12 unusu alfajiri na walikuwa wakisubiri kuabiri ndege wakati Fatuma alipozirai. Omari amesema Fatuma amepata nafuu hospitalini na familia yake imeomba kufanyiwa uchunguziA� ili kubainisha sababu ya kuzirai kwake. Omari amesema mteja wake hakuonyesha dalili zozote za kuwa na msongo wa mawazo na alikuwa mchangamfuA� . Omari amesema hawataweza kuhudhuria mazishi hayo jinsi walivyotumainia kutokana na kisa hicho. Ramadhan alikuwa amewasilisha kesi ya kuzuia mazishi ya Too akisema alikuwa baba ya mtoto wake ambaye anadai ametengwa kushiriki kwenye mazishi hayo.