Mawaziri watetea serikali ya Jubilee dhidi ya shutuma kutoka upinzani

Mawaziri watatu wameitetea vikali serikali ya A�Jubilee A�dhidi ya shtuma kutoka kwa A�upinzani kwamba imeshindwa A�kutekeleza ahadi A�katika manifesto yake A�. Waziri wa A�elimu Dkt , Fred Matianga��i , mwenzake wa ugatuzi A�Mwangi Kiunjuri na mwenzao wa kawi Charles Keter walitaja shtuma hizo kuwa A�propaganda A�nakuwahimiza wapiga kura kuzipuuza propaganda hizo. Mawaziri hao walitaja miradi kadha wa kadha iliyotekelezwa na serikali ya Jubilee na kuitaja kuwa ushahidi ambapo wakosoaji hao hawaoni . Walikuwa wakiongea katika uwanja wa shule ya msingi ya Nyambera wakati wa mchango wa kusaidia mradi wa ujenzi wa A�kanisa A�ya parokia ya Kisii mjini . Akiwaongoza watatu hao, Matiangi alisema baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakieneza uongo dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na utendakazi wa serikali yake na kuitaja sekta ya elimu. Alielezea kuwa zaidi ya asilimia 70 ya maendeleo yamepatikana kutoka shule ya msingi hadi ya upili na ada za mitihani za milioni 1.6 kulipiwa bila kujali wamiliki wa shule mwaka huu. A�