Mawaziri kushiriki mahojiano ya huduma ya serikali kwenye radio

Mawaziri kuanzia leo Alhamisi wataanza kushiriki katika mahojiano kupitia redio kuangazia utoaji huduma wa serikali ya Jubilee. Mawaziri hao watakuwa katika vituo mbali mbali vya redio katika mahojiano yatakayoanza mwendo wa saa 7.30 asubuhi hadi saa mbili asubuhi. Wananchi wameshauriwa kuwauliza maswali katika mitandao ya kijamii kwa kutumia hash tag #GOKDelivers. Haya yanajiri huku serikali ya Jubilee ikishinikiza kufanyiwa marekebisho sheria za uchaguzi za mwaka 2016 ili iweze kufanya kampeini kupitia mitandao ya kijamii kabla ya uchaguzi mkuu ujao . Katika mswada wa marekebisho uliowasilishwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la taifa Aden Duale, kipengee katika sheria hizo kinachoizuia serikali kutangaza ufanisi wake kupitia mitandao ya kijamii katika mwaka wa uchaguzi kitaondolewa . Serikali ya Jubilee inasema kuwa kipengee hicho kinakiuka katiba kwasababu kinawanyima wakenya fursa ya kupata habari za serikali.