Mawakili kuandamana kupinga ukiukaji wa sheria na maagizo ya mahakama

 

Mawakili sasa watafanya maandamano alhamisi wiki hii wakitaka wakenya wote waheshimu sheria. Mawakili walikuwa wamepanga kususia kutoa huduma zao kuanzia leo lakini chama cha wanasheria hapa nchini kikaahirisha mgomo huo kikisema wanachama wake watahudhuria vikao vyote vya mahakama wakiwa wamejifunga tepe za njano kuashiria mwanzo wa kususia utoaji huduma kama hatua ya kulalamika kuhusu mtindo unaoendelea wa kuto-tii sheria na maagizo ya mahakama. Kampeni hiyo ya utepe wa njano itaendelea hadi pale watu watakapoanza kuafiki sheria. Taarifa hiyo imeongeza kuwa mawakili hao watawashtaki maafisa wakuu serikalini na wale wa uma wasioz-ngatia sheria. Chama cha LSK kilikuwa kimepanga kuanza mgomo wa wanachama leo kote nchini isipokuwa tu wanachama wanaoshughulikia rufaa za uchaguzi ambazo sharti zitatuliwe haraka.