Mauaji ya Chris Msando yaendelea kuibua hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi

Mauaji ya meneja wa ICT katika tume ya IEBC Chris Msando, yanaendelea kuibua hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi wa tabaka mbali mbali. Mbunge wa Bahati, Kimani Ngunjiri amehimiza polisi kuharakisha uchunguizi wao kuhusiana na mauaji ya Msando. Seneta wa A�Makueni, Mutula Kilonzo Junior alitaja kifo cha Msando A�kuwa mauaji , akiongeza kwamba wakenya wanapaswa kulipatia swala hilo uzito kamili. Aliunga mkono wito wa kuwapatia ulinzi maafisa wa tume ya IEBC na pia vifaa vya tume hiyo usiku na mchana. Mwili wa Msando A�ambao ulipatikana kichakani katika eneo la Muguga huko Kikuyu, Kaunti ya Kiambu, ulitambuliwa Jumatatu na watu wa familia yake kwenye hifadhi ya maiti ya City baada ya kuripotiwa kutoweka kwa muda wa siku tatu. A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�A�