Matumaini Ya Rais Wa Bolivia Kuchukua Hatamu Mara Ya Nne Yadidimia

Matokeo ya muda ya kura ya maamuzi nchini Bolivia yanaonesha kuwa rais Evo Morales ameshindwa katika juhudi zake za kutaka kuwania kwa mara ya nne uongozi wa nchi hiyo wakati kipindi chake cha sasa kitakapokamilika.Huku asilimia 82 ya kura ikiwa imehesabiwa,ilidhihirika kuwaA� wale wanaopinga katiba ya nchi hiyo kufanyiwa marekebisho wanaongoza kwa aslimia A�8.4 ya alama. Morales ambaye ni A�rais wa kwanza mzawa wa A�taifa hilo alisema ataheshimu kauli ya raia,licha yaA� kuyashutumu mashirika yasipendelea mabadiliko kwa kuendesha vita viovu dhidi ya swala hilo.Morales ambaye ni mzaliwa wa jamii ya Aymara na mkulima maarufu wa A�zao la cacao,alishika hatamu za uongozi wa taifa hilo mnamo mwaka 2006.Kipindi cha utawala cha Morales kinamalizika mwaka 2020.Ikiwa katiba ya nchi hiyo ingefanyiwa marekebisho basi A�ingemwezesha Morales kuwania tena wadhifa wa urais mwaka wa 2019 na hivyo kusaliaA� mamlakani hadi mwaka wa 2025. Upinzani umefurahia matokeo hayo ya muda,ambapo wameelekea katika miji mbali mbali nchini humo kusherehekea jambo hilo