Matokeo Ya Mtihani Wa KCSE Kutangazwa Alhamisi Ijayo

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE- yatatangazwa alhamisi wiki ijayo. Waziri wa elimu Sayansi na Takenolojia Dr. Fred Matianga��i ataongoza hafla ya kutangazwa kwa matokeo hayo katika Jumba la Mitihani Jijini Nairobi. Kwenye taarifa kwa waandishi wa habari, mkurugenzi mkuu wa baraza la kitaifa la mitihani, Joseph Kivilu alisema watahiniwa wataweza kupata matokeo yao kwa kutuma ujumbe mfupi wa nambari yao ya Index kwa 22252 punde baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo