Matokeo ya KCPE yatangazwa

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane mwaka huu KCPE yametangazwa. Matokeo hayo yalitangazwa leo asubuhi na waziri wa elimu Dr Fred Matianga��i. Matianga��i alisema matokeo ya mtihani huo mwaka huu yameboreka. Alitangaza kuwa mwanafunzi bora zaidi amepata alama 455 kati ya alama zoteA� 500. Mwanafunzi bora zaidi mwaka uliopita alipata alama 437. Matokeo ya mwaka huu yameborekwa kwa masomo yote. Zaidi ya wanafunzi 900 wamepata zaidi ya alama 400 kwenye mtihani huo. Matianga��I amesema amefurahishwa na matokeo ya wanafunzi wa shule za msingi za umma akisema mwanafunzi wa pili bora zaidi ni wa shule ya umma. Hata hivyo amesema wanafunzi hao hawakufanya vyema katika masomo ya sayansi na masomo maalum. Alisema serikali sasa itaangazi juhudi za kuboresha matokeo ya masomo hayo mawili. Waziri amesema serikali inatilia maanani swala la kushirikiana na wadau wote ili kubuni mazingira bora kwa wanafunzi kusoma. Kaunti za Kakamega na Trans Nzoia zilifanya vyema kulingana na Matianga��i. Akiwahutubia maafisa wa elimu alisema mizozo ni sharti iepushwe katika sekta ya elimu. Amewashukuru walimu wote wakuu na wazazi kwa kutia bidii kuhakikisha watoto wanafanya mitihani ya kitaifa. Wakati huo huo waziri amewatahadharisha wale wanaolenga kuharibu musatakabali wa watoto kwa kuvuruga mitihani ya kitaifa. Wanafunzi sasa wanaweza kupata matokeo yao kwa kutuma nambari zao za usajili kwa nambari 22252. Matokeo hayo yametangazwa mwezi mmoja kabla ya muda wa mwaka uliopita