Matiang’i kukutana na wadau, sekta ya elimu

Waziri wa Elimu Dr. Fred Matianga��i leo anatarajiwa kukutana na wadau wa sekta hiyo, ili kujadili njia mwafaka ya kutekeleza mtaalaA�A�mpya wa masomo, ambao tayari umezinduliwa. Haijabainika wazi iwapo mkutano huo utahudhiriwa pia na waakilishi waA�A�chama cha kitaifa cha waalimu – (KNUT), na kile cha waalimu wa shule za sekondari na vyuo (KUPPET). Msimamo wa vyama hivyo viwili umekuwa wa kukosoa mtaala mpya wa masomo vikisema uliharakishwa bila kushirikisha wadau wa sekta hiyo. Aidha, vyama hivyo vimetishiaA�A�kuichukulia serikali hatua za kisheria, ama kuitisha mgomo, iwapo serikali haitaahirisha mapendekezo yaliyomo kwenye mtaala mpya wa masomo.

Akihutubia mikutano ya wakuu wa shule hivi majuzi, katibu mkuu wa KNUT Wilson Sosion, alisema vifaa vya masomo kwa mtaala mpya havijafanyiwa majaribio, wala mafunzo kutolewa kwa waalimu. Sosion alisema hatua hiyo inafanya iwe vigumu kutekeleza mtaala mpya wa masomo kuanzia mwezi huu wa Januari.A�A�Waalimu walisema utekelezaji kiholela wa mfumo wa elimu wa 2-6-3-3-3 huenda ukasambaratisha hatua zilizopigwa chini ya mfumo wa elimu waA�A�8-lakini serikali ilipuuzilia mbali hoja hizo kama zisizokuwa na msingi, ikisema kwamba uchunguzi wa mtaala mpya umechukua miaka 14 na kwamba muda wa utekelezaji wa mtaala mpya umetanuliwa hadi mwaka 2020.