Matianga��i azindua halmashauri ya taifa kuhusu viwango na uthibiti wa elimu ya vyuo vikuu

Waziri wa elimu Fred Matianga��i jana alizindua halmashauri ya taifa kuhusu viwango na uthibiti wa uhitimu wa elimu ya juu ambayo itakabidhiwa jukumu la uthibiti wa viwango vya aina zote za uhitimu katika vyuo vikuu. Halmashauri hiyo mpya itajukumiwa kuratibu viwango vya uhitimu jukumu ambalo kwa sasa linatekelezwa na tume ya elimu ya vyuo vikuu. Akiongea wakati wa uzinduzi huo, mwenyekiti wa halmashauri ya kuwianisha viwango vya elimu Bonventure Wanjala alisema halmashauri hiyo pia itaratibu mfumo wa kutoa vyeti vya uhitimu kwa shahada zinazotolewa na vyuo vikuu na pia kukabiliana na utoaji vyeti bandia.Majukumu ya halmashauri ya uhitimu nchini pia yatajumuisha ustawishaji sera kuhusu uhitimu, mfumo wa utoaji vyeti na ule wa kutathmini vyeti hivyo. Majukumu mengine yatajumuisha uzinduzi wa takwimu ya taifa ya uhitimu, uchapishaji nambariA� na maongozi ya uhitimu, utoaji ripoti ya kila mwaka kuhusu mfumo wa uhitimu na pia kufanya mashauri na wadau wote katika sekta hiyo.Ni matumaini kwamba halmashauri hiyo mpya itakabiliana na hali za utata ambazo huzuka mara kwa mara kuhusu uhitimu wa watu wanaotaka kuhudumu katika nyadhifa za juu kwenye utumishi wa umma na pia kwenye nyadhifa za kisiasa. Mwaka huu wa uchaguzi wawaniaji kadhaa wa nyadhifa za kisiasa uhitimu wao kimasomo ulizua shaka na halmahauri hii inadharimia kuhakikisha hali za kutatanisha kama hizo hazijiri siku za usoni.