Matianga��i awaonya waalimu wakuu watakaofuja fedha za lishe shuleni

Waziri wa elimu Dr. Fred Matianga��i amewaonya waalimu wakuu wa shule na bodi zao kwamba wamo hatarini ya kuhukumiwa vifungo gerezani wakifuja fedha za mpango wa kutoa lishe shuleni. Akiongea alipofungua mkutano wa muungano wa Afrika na shirika la mpango wa chakula duniani, Matiangi alisema kwamba serikali imeimarisha mpango huo kwa lengo la kuutekeleza katika shule zote za umma ili kuhakikisha watoto wote waliohitimu umri wanakwenda shuleni. Alilaumu ufisadi na urasimu mwingi kwa kuchelewesha utekelezaji mpango huo katika shule kadhaa kote nchini akionya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaopatikana wamefuja fedha za mpango huo.Kadhalika Matianga��iA� aliyahimiza mataifa ya kiafrika kutenga rasilimali zaidi kwa mipango ya kutoa lishe shuleni iwapo kanda hii inatarajiwa kustawi.