Matianga��i, awahakikishia wakenya usalama wakati wa marudio ya uchaguzi

Waziri wa usalama Fred Matianga��i, amewahakikishia wakenya kwamba maafisa wa usalama wako tayari kwa marudio ya uchaguzi wa urais, ambapo aliwaonya wanasiasa wanaowachochea wakenya kwamba watashtakiwa. Aidha Matiangi aliwaonya wakuu wa muungano wa NASA dhidi ya kuhujumu mfumo wa kiusalama waliopewa, akisema uamuzi wa kuondolewa kwa baadhi ya maafisa ni wa mwisho. Akiongea huko Kajiado alikokutana na maafisa wa usalama kutoka kaunti za Kajiado na Narok, waziri huyo alitofautiana na kiongozi wa NASA, Raila Odinga na akamhimiza kutumia utaratibu wa sheria kuwaondoa watumishi wa umma mamlakani badala ya kuitisha maandamano. Matianga��i alisema matamshi ya wanasiasa yatafuatiliwa kwa makini na watakaopatikana na hatia watashtakiwa.