UASU lataja agizo la Matiang’i kuhusu mishahara kuwa lenye nia mbaya

Agizo la waziri wa Elimu A�Fred Matiangi kwamba wasimamizi wa vyuo vikuu vya umma wasimamishe mfumo wa A�kuwaajiri wafanyakazi kwa kuwapa kazi za kudumu na pia A�marupurupu ya baada ya A�kustaafu limetajwa kuwa lenye nia mbaya . Chama cha Wahadhiri A�wa Vyuo Vikuu vya Umma (UASU) kimetisha kwenda mahakamani A�iwapo agizo hilo A�litageuzwa kuwa sera. Katibu Mkuu wa chama cha A�Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma Constantine Wasonga amesema A�hatua ya A�Matiaga��i A�itachangia wahadhiri kuhamia mataifa mengineA� A�na hatimaye kuvurugha sekta ya elimu ya juu hapa nchini. A�Alisema wanapinga sekta hiyo A�kuendeshwa kupitia amri. A�Chama cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu Nchini kilikuwa kimesema kwamba agizo hilo litatiza mazingira ya kazi. Kwenye Mkutano A�na manaibu wa Machancella wa vyuo vikuu katika A�taasisi ya Masomo ya Fedha Nchini (SMS), Matiangi A�alisema mnamo siku zijazo wafanyakazi wa vyuo vikuu watastahili kuajiriwa kwa kandarasi