Matiang’i Ashauri Wanafunzi Kuzingatia Utaratibu Ili Kutatua Mizozo

Waziri wa elimu dkt. Fred Matianga��i amewashauri wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotofautiana na wasimamizi wa vyuo vyao kutumia utaratibu uliopo kikamilifu kutatua hali hiyo kabla ya kuwasilisha malalamishi kwa wizara yake.A� Waziri huyo wa elimu alisema kwa mfano wanafunzi wanaotimuliwa vyuoni na hawajaridhishwa na hatua hiyo, wanapaswa kuwasilisha malalamishi yao kwa baraza la vyuo vikuu kwanza. Akiongea katika shule ya upili ya Gathuthuni katika kaunti ya Kirinyaga, waziri huyo alisema licha ya malalamishi ya wanafunzi hao kuwa halali, wizara yake haiwezi kusaidiaA� hasa pale wanafuzi walioathiriwa wamekosa kuzingatia utaratibu. Alisema vyuo vikuu ni taasisi huru na hivyo wizara yake haiwezi kuingilia kati haraka maswala ya vyuo hadi pale swala hilo litakapowasilishwa katika afisi yake kwa kuzingatia taratibu zinazofaa. Matianga��i alikuwa akijibu maswali ya vyombo vya habari kuhusu hatma ya wanafunzi 45 wa chuo kikuu chaA� Kirinyaga waliosimamishwa. Wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa kwanza hadi wa nne walisimamishwa kwa miaka minne kila mmoja kwa kususia masomo wakilalamikia kuongezwa kwa karo bila kuwaarifu wazazi wao.