Serikali kushinikiza Kiswahili kuwa somo la lazima

Waziri wa Elimu Dr. Fred Matiangi amesema wizara yake itashinikiza kudumishwa kwa Kiswahili kuwa somo la lazima katika mtaala mpya wa elimu. Matiangi anadai kwamba Kiswahili ni lugha muhimu katika kuimarisha umoja katika jumuiya ya Afrika mashariki na hivyo basi ipo haja ya kuzingatia kudumishwa kwa somo hilo. Waziri pia alisema ataiongoza nchi hii kushinikiza kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano yote ya Jumuiya ya Afrika mashariki EAC kufanywa kuwa sheria.A� MatiangiA� alikuwa akiongea wakati wa kuzinduliwa kwa kamusi ya Kiswahili ya Longhorn, ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika taasisi ya maendeleo ya mitaala ya masomo nchini a��KICD.