Matiang’i afurahia idadi ya wasichana waliofanya mtihani wa KCPE

Waziri wa elimu Dr. Fred Matiang’i amepongeza hali ya kuongezeka pakubwa kwa idadi ya wasichana waliofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kulingana na  Matiang’I amesema  idadi ya  wasichana imekaribiana na ile  ya wavulana waliofanya mtihani huo mwaka huu. Amesema asilimia 50.19 ya watahiniwa wote waliosajiliwa walikuwa wavulana huku asilimia 49.81 wakiwa wasichana. Matiangi vile vile ametaja kaunti 27 miongoni mwao Meru, Kakamega, Murang’a na Nakuru miongoni kaunti nyingine ambazo zimenakili idadi kubwa ya wasichana kuliko wavulana.Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la kitaifa la mitihani hapa nchini KNEC George Magoha amesifu hali hiyo ya idadi ya wavulana kukaribiana nay a wasichana na kutaja kuwa hatua kubwa katika kumpa uwezo mtoto wa kike.