Matiang’i Alaumu Muingilio Wa Kisiasa Kwa Kuathiri Viwango Vya Elimu

Waziri wa elimu Dr. Fred Matianga��i amependekeza kuwa manaibu wa machansela wa vyuo vikuu wawe wakisailiwa kabla ya kuteuliwa rasmi. Dr. Matianga��i alisema jopo la uteuzi linalojumuisha chansela, baraza kuu na viongozi wa wanafunzi wa chuo mahsusi pamoja na wasomi wa zamani wa chuo hicho linapaswa kuwasaili wawaniaji wa nyadhifa hizo kabla ya kuteuliwa kwao rasmi. Alisema hatua hiyo itahakikisha utaratibu wa kuwateua manaibu wa machansela unafanywa kwa njia iliyo wazi. Dr. Matianga��i alisema hili ni baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa wakati wa majadiliano kuhusu sera, kanuni na viwango vya elimu katika vyuo vikuu hapa nchini. Waziri aliwahimiza wasimamizi wa vyuo vikuu kubuni mikakati ya kusuluhisha mizozo badala ya kutafuta utatuzi mahakamani. Aidha alisema muingilio wa kisiasa katikasekta ya elimu ya juu umeathiri uwezo wa vyuo hivyo wa kubuni na kudumisha miundo mbinu inayohitajika ili kuboresha viwango vya elimu hapa nchini.