Matiang’i akutana na maafisa wakuu wa usalama

Kaimu waziri wa usalama wa ndani, Dr Fred Matianga��i anakutana na maafisa wakuu wa usalama kwenye taasisi ya mafunzo ya utawala wakati taifa hili likijiandaa kwa marudio ya uchaguzi wa urais. Mkutano huo unatarajiwa kujadili mikakati ya kuimarisha usalama wakati na baada ya uchaguzi huo unaojiri wakati mihemko ya kisiasa ikikumba taifa hili. Serikali imewahakikishia Wakenya kuwa usalama utaimarishwa siku ya Alhamisi na kutahadharisha wanaonuia kuzua fujo kuwa watakabiliwa vilivyo. Muungano wa Dr Fred Matianga��i umewahimiza wafuasi wake kutoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa madai kuwa mfumo wa uchaguzi humu nchini una dosari.