Matiang’i Akiri Teknolojia Ilichangia Ubora Wa Mitihani

Serikali imesema kwamba marekebisho ya haraka ya usalama wa makaratasi ya mitihani ya kitaifa ya mwaka uliopita na utoaji haraka wa matokeo A�ya mitihani hiyo ulitokana na matumizi ya mifumo ya teknolojia ya kisasa ya habari na mawasiliano.Waziri wa elimu Dr. Fred Matianga��i amesema serikali ilitekeleza marekebisho kadhaa kwenye usimamizi wa mitihani ya kitaifa kwa kuanzisha vituo 25 vipya jijini Nairobi vya teknolojia ya kisasa ya mawasiliano kwa usaidizi wa wizara ya habari na teknolojia ya mawasilano.Akiongea jana katika shule ya mafunzo ya serikali wakati wa sherehe ya kufuzu kwa wanafunzi wa uhandisi na wanagenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano chini ya mpango wa Rais wa ustawishaji wa vipaji vya dijitali, Dr Matiangi alisema uwekezaji wa pesa raslimali nyingi katika ustawishaji wa teknolojia ya habari na mawasilano hapa nchini umeleta manufaa kwa kuwezesha kuchunguzwa kwa usalama wa mitihani kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuwezesha matokeo kutolewa haraka. Dr Matiangi alisema serikali inatumia teknolojia kukabiliana na vitendo viovu miongoni mwa jamii na kuimarisha huduma ya uma kwa wakenya. Waziri wa gteknolojia ya habari na mawasiliano Joe Mucheru alisema serikali inapanua mitandao ya mawasiliano ya kidijitali hapa nchini ili kuimarisha huduma na kutoa nafasi zaidi za kazi.