Mathias Momanyi

MAELEZO / MUHTASARI

Yeye ni produsa mwandamizi, mtangazaji na mlezi wa makala mbalimbali ya Kiswahili kituoni KBC Radio Taifa. Amehitimu kwa shahada ya uanahabari kutoka chuokikuu cha Moi. Fauka ya uanahabari, Mathias Momanyi ni mwalimu na mwandishi wa vitabu kadhaa vya Kiswahili ambavyo hutumika nchini katika shule za msingi kwa idhinisho la Taasisi ya ukuzaji mitaala nchini KICD. Ana pia stashahada ya mawasiliano na uanahabari kutoka chuokikuu cha MKU.

VIPINDI:

VUVUZELA ( Saa mbili usiku hadi saa sita usiku ) a�� Huenda hewani kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi kwa ushirikiano wa mwanahabari mwenzaA�Hoka wa Mwahoka.

RAMANI YA KISWAHILI (Jumamosi saa kumi na mbili hadi saa nne asubuhi) a�� Kipindi cha kuelimisha kuhusu lugha yetu tukufu ya Kiswahili nchini chini ya katiba iliyorasmishwa mwaka elfu mbili na kumi. Kina wafuasi takriban 27,000 elfu katika mtandao wa jamii ya Facebook.

KAULIMBIU: a�?Binadamu hali sifa akashiba .a�?

Wasiliana naye: @mathiasmomanyi

Facebook: Double M. A� Mathias Momanyi

Mathias Momanyi