Mathew Lempurkel asema maisha yake yamo hatarini

Mbunge wa Laikipia kaskazini Mathew Lempurkel amesema maisha yake yamo hatarini. Akiongea na wanahabari katika hoteli moja mjini Maralal, Lempurkel alisema alipokea ujumbe wa kutishia maisha yake kwenye rununu yake kutoka kwa nambari ya simu asiyoifahamu na punde tu baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa NASA mjini Maralal. Alisema ujumbe huo ulisema kwamba atakatwa kichwa. Ameihimiza serikali iimarishe usalama wake wakati huu wa kampeini za uchaguzi kwa sababu ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa wote.