Mathare United yashajili Mlinzi Gilbert Osonga kutoka Posta Rangers

Kilabu cha Mathare United kinachoshiriki katika ligi ya Sportpesa humu nchini kimemsajili mlinzi Gilbert Osonga kutoka Posta Rangers. Mlinzi huyo ametia saini mkataba wa miaka minne na kilabu hicho.Osonga, aliyezichezea timu za Chuo kikuu cha Zetech na Young Rovers atajumwika na nahodha wa Mathare George Owino na Andrew Juma katika safu ya ulinzi timuni. Osonga sasa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na kilabu hicho msimu huu wa usajili.