Matayarisho ya mitihani ya KCPE, KCSE yakamilika

Matayarisho ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu ya darasa la nane  KCPE na ya kidato cha nne KCSE yamekamilika. Mwenyekiti wa baraza la mitihani ya kitaifa NEC George Magoha amethibitisha kwamba wamekagua makasha yote 459 yatakayotumiwa kuhifadhi vifaa vya mitihani hiyo na kudhibitisha vifaa hivyo vya mitihani vitakuwa salama wakati wa kipindi chote cha mitihani hiyo.

Akiongea wakati wa ziara ya ukaguzi wa makasha hayo katika kaunty ndogo ya Langatta, kaunty ya Nairobi,Prof. Magoha alionya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaouza makaratasi bandia ya mitihani ya kitaifa kabla ya mitihani hiyo kufanywa.Alielezea masikitiko yake kwamba baadhi ya wanafunzi na wazazi tayari wametapeliwa licha ya baraza hilo kuhakikishia uma kwamba mitihani yote ya kitaifa iko salama.

Katibu katika wizara ya elimu,Dr. Belio Kipsang,ameonya kwamba kituo chochote cha mitihani hiyo kitakachoifungua kabla ya wakati wake wa kufanywa kuwadia kitafungwa mara moja na kutangazwa kuwa eneo lla uhalifu.katibu kadhalika alisema watahiniwa watakuwa na siku za maombi lakini akaonya kwamba hapana mtu yeyote kutoka nje ataruhusiwa shuleni wakati wa maombi hayo.