Matakwa ya chama cha wauguzi nchini kwa SRC

Chama cha wauguzi nchini kimeitaka tume ya ukadiriaji mishahara na marupurupu kuondolea mbaliA� mara moja arifa ya ukadiriaji wa mishahara ya watumishi wa umma kikisema kuwa wauguzi hawakuzingatiwa ipasavyo. Katibu mkuu wa chama hicho Seth Panyako alisema arifa hiyo ya tarehe moja mwezi huu iliwapandisha vyeo maafisa wa ngazi za juu huku ikiwashusha ngazi wauguzi wa ngazi za chini. Chama hicho kimeapa kuwasilisha kesi mahakamaniA� kulalamikia hatua hiyo ya tume ya ukadiriaji mishahara huku ikitaka tume ya kuwaajiri watumishi wa umma kuingilia kati. Panyako ametoa wito kwa katibu mkuu wa muungano wa Cotu Francis Atwoli kushughulikia mzozo huo wa sekta ya afya, la sivyio chama hicho kijiondoe kutoka muungano wa Cotu. Wauguzi hao wameamua kusimama kidete licha ya vitisho vya kuwafuta kazi.