Mashirika ya kimataifa ya ndege kubadili safari zake baada ya onyo kuwa huenda ndege zikashambuliwa

Mashirika ya kimataifa ya ndege za abiria yamesema kwamba yanajaribu kubadili safari zake baada ya halmashauri moja ya usalama wa angani huko Ulaya kuonya kwamba huenda ndege za abiria zikashambuliwa zitakapokuwa zikipaaa juu ya anga ya Syria mnamo siku zijazo.Halmashauri ya ulaya ya usalama wa safari za ndege imeyatahadharisha mashirika ya ndege za abiria kwamba kunaA� uwezekano wa ndege zao kushambuliwa kwa makombora ya kutungua ndege mnamo kipindi cha saa 72 zijazo na kuzitaka zichukue hatua za dharura.

Shirika la ndege la Ufaransa-Air France ni miongoni mwa yale ambayo tayari yamebadili njia zake,hasa safari za kwenda Beirut na Tel Aviv,huku shirika la ndege za mashariki ya kati likibadili safari za ndege zake zinazosafiri hadi Beirut,nchini Lebanon.Safari za ndege kuelekea mataifa ya ghuba pia zimebadilishwa na kucheleweshwa kwa muda wa dakikaA� 30 hadi 40,kwa kuwa badala ya kupitia juu ya anga ya kaskazini mwa SyriaA� zitapitia eneo la Sinai huko Misri hadiA� nchi za Ghuba.