Mashirika Ya COTU Na NSSF Kukutana Kwa Majadiliano

COTU

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini, (COTU), hazina ya malipo ya uzeeni (NSSF) na wizara ya leba zimezozana kuhusiana na uamuzi wa kutupilia mbali kesi zinazoendelea mahakamani huku muungano wa COTU ukiishtumu serikali kwa A�kunuia kutumia pesa za NSSF kufadhili kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2017.

Naibu katibu mkuu wa COTU Benson Okwaro alidai kwamba serikali inajaribu kuwashawishi kutupilia mbali kesi hiyo ili kuwezesha kutekelezwa kwa ada mpya zitakazowezesha kukusanywa kwa kiasi kikubwa cha pesa za kufadhili kampeni za serikali.A� Hazina yaA� NSSF iliongeza ada zake mwaka 2013 ili wanachama wachange zaidi huku wafanyikazi na waajiri wakichanga asilimia sita ya mshahara wa wafanyikazi kwenye hazina hiyo. Hata hivyo hatua hiyo ilipingwa mahakamani na COTU na shirikisho la waajiri nchini na baadaye ikasimamishwa.

Kwa sasa wafanyikazi wanachanga shilingi 200 kwa NSSF. Okwaro alisema kwamba mbinu zinazotumiwa na serikali zilitumiwa na tawala zilizokuwepo na hazitafaulu sasa. Alisema kuna makundi yanayosubiri kesi hiyo itupiliwe mbali ili kuthibiti hazina hiyo. Mwenyekiti wa bodi ya wathamini wa hazina ya NSSF Gideon Ndambuki akiongea mjini Mombasa siku ya Jumatatu, aliiomba COTU kutupilia kesi hiyo na kukomesha mzozo huo. Okwaro alitoa wito wa mashauriano ya kutosha kama sehemu ya shinikizo zilizotolewa kabla ya kesi hiyo kuondolewa.