Mashindano ya wanariadha wasiozidi miaka 18 yaanza rasmi Kasarani

George Manangoi mdogowe, Elijah Manangoi ambaye ni mshindi wa nishani ya fedha katika mbio za mita 1,500 katika mashindano ya riadha duniani ya mwaka 2015 jijini Beijing,Uchina alishinda katika mchujo waA� kwanzaA� kwa muda wa dakika tatu na sekunde 55.00. Belete MekonenA� wa Ethiopia na Kiprop Daniel wa Uganda walimaliza katika nafasi za pili na tatuA� mtawalia. Dominic Kipkemboi alishinda katika muda wa dakika tatu na sekundeA� 48.77 licha ya kuhisi maumivu baada ya kuumia mazoezini huku akitarajia kupona kabla ya fainali Jumapili hii. Wakati huo huo, mvulana wa pekee anayewakilisha Kenya katika mbio za mita mia moja, Elijah Matayo alifuzu kwa nusu fainali ya mbio hizo baada ya kumaliza wa tatu ambapo mshindi alikuwa Tyriek Wilson wa Jamaika. Denilson Mahatiure wa Jamhuri ya Dominican alimaliza wa pili. Aidha, mbio zinazosubiriwa mno ni fainali ya akinadada ya mita elfu tatu ambapo wakenya na Waethiopia wataendeleza ukinzani wao.Bingwa wa dunia katika mbio za mita elfu 5 Emaculate Chepkirui atamwongoza Beatrice Chebet fainalini kuchuana na Waethiopia watakaoongozwa na mshindi wa nishani ya fedha Barani Afrika kwa Mentu Ketema na Abersh Minsewo. Wanariadha wa Bara Afrika wametwaa ushindi kutoka mbio hizo tangu zilipobuniwa mwaka 1999. RaisA� Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuyanzisha rasmi mashindano hayoA� yanayowashirikisha wanariadha kutoka mataifa 120 alasiri hiiA� uwanjani Kasarani.