Mashindano ya mbio za magari ya langalanga kutolewa kwa ratiba ya Malaysia

Msururu wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga hautajumuisha mashindano ya Malaysia msimu ujao, baada ya kuondolewa kwenye ratiba ya mbio hizo.

Umuzi huo uliotangazwa na afisa mkuu wa mauzo wa mashindano hayo Sean Bratches, unawadia baada ya serikali Malaysia kutilia shaka manufaa ya mashindano hayo kwa taifa hilo. Sean Bratches alisema mashindano ya mwaka ujao yatajumwisha mikondo 21 licha ya kutokuwapo kwa mashindano ya Malaysia. Mkondo wa Ufaransa utarejea mwaka ujao kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka kumi, sawa na mashindano ya Ujerumani yatakayorejea baada ya kutoandaliwa msimu huu. Msururu huo wa Malaysia haukuwavutia mashabiki wengi katika misimu ya hivi majuzi. Mashindano ya mwaka huu yataandaliwa mwezi Septemba, jijiniA´┐Ż Sepang.