Maseneta waapa kufuatilia marekebisho muhimu katka sekta ya elimu

Maseneta wameapa kufuatilia marekebisho muhimu ya elimu ili kuiboresha katika taasisi za elimu humu nchini. Wakiongea wakati wa ziara ya shule mbali mbali katika kaunti ya Uasin Gishu maseneta hao walizitaka serkali za kaunti kutoa fedha zaidi kwa elimu ya chekechea ili kubuni mazingira bora ya masomo kwa watoto.

Maseneta hao waliokamilisha vikao vyao katika kaunti ya Uasin Gishu walitetea hatua hiyo wakisema imewaokolea wananchi mamilioni ya pesa za marupurupu ya kamati. Kamati ya elimu ya bunge la seneti iligundua kwamba shule nyingi katika kaunti ya Uasin Gishu hazina miundo mbinu kwa watoto walio na mahitaji maalum.

Kwa wakati huu Kenya haina utaratibu wa kisheria unaotoa mwongozo wa ujenzi wa vituo vya elimu ya chekechea. Hata hivyo maseneta waliahidi kubuni sheria itakayotoa utaratibu muhimu kwa elmu bora katika shule za humu nchini.

Pia maseneta hao walitoa wito wa kuwacha kuwabagua watoto wanaoishi na ulemavu na wakawahimiza wazazi kuwapeleka shuleni watoto walio na mahitaji maalum. Wabunge wa seneti walifanya vikaa wiki hii katika kaunti ya Uasin Gishu ambavyo ni vya kuwanza kufanuwa nje ya jiji la Nairobi tangu kuzinduliwa kwa katiba mpya hapo mwaka wa 2010.