Mario Balotelli Arejea Katika Kilabu Cha Liverpool

Mario Balotelli alirejea katika kilabu cha Liverpool jana huku kocha wa kilabu hicho Jurgen Klopp akianzisha rasmi mazoezi ya kujiandaa kwa ubingwa wa A�ligi kuu ya soka nchini Uingereza, msimu ujao. Wachezaji wapya Sadio Mane, Joel Matip, Loris Karius na Marko Grujic wote walifanya mazoezi uwanjani A�Melwood pamoja na wachezaji ambao hawakuwakilisha mataifa yao katika michuano ya Bara Ulaya. Baloteli ambaye alikuwa kiungo wa timu za Inter Milan na Manchester City, alifunga bao moja pekee kati ya mechi 23 alizocheza msimu uliopita wa ligi kuu ya soka nchini Italia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kuondoka Liverpool msimu huu kwani nia za kumsajili zimezagaa kutoka mataifa ya Uturuki na China majuma machache yaliyopita. Aidha, Liverpool itamenyana na timu za Chelsea, AC Milan, Roma na Baselona katika mechi za kujipima nguvu kabla ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza kuanza ambapo itafungua dimba dhidi ya Asenali A�tarehe 13 mwezi Agosti