Margaret Kenyatta atembelea familia zilizoathiriwa na baa la njaa Marsabit

Mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta jana alitembelea familia zilizoathiriwa na baa la njaa katika eneo la Horr Kaskazini, Kaunti ya Marsabit ili kujifahamisha zaidi na hali ilivyo, na pia kuungana na maafisa wa shirika la msalaba mwekundu katika usambazaji wa fedha za misaada. Mama wa taifaA� alikizuru pia kituo cha afya cha Horr Kaskazini,A� ambako alishuhudia wanawake na watoto wakifanyiwa uchunguzi wa kubaini hali ya utapia mlo kufuatia uhaba wa chakula ambao umetokana na hali ya ukame. Viwango vya utapia mlo ni asilimiaA� 30 kwenye kaunti ya Marsabit, na asilimia 34 katika Kaunti ndogo ya Horr Kaskazini. Baada ya kujifahamisha na athari kamili na pia kiwango cha ukame sawia na mgogoro wa chakula kwenye kaunti hiyo, Mkewe Rais alisema kwamba afisi yake itajitahidi kupunguza mateso ambayo yamesababishwa na ukosefu wa chakula cha kutosha.Alitoa mchango wa gari la pili la huduma za Kiliniki kwa Kaunti hiyo ya Marsabit ili kuongezea gari lililoko sasa ambalo linahitajika kuhudumiaA� kaunty hiyo kubwa ya eneo la kilomitaA� 75,750 mraba.A� Akiandamana na Mama wa taifa , Gavana wa Kaunti ya Marsabit Ukur Yatani alipongeza juhudi zake kupitia kwa kampeini ya Beyond Zero, akisema wanawake wengi na pia watoto wamenufaika na mtadi huo.Kati ya Kaunti 23 ambazo zimeathiriwa na hali ya ukame,kaunti ambazo zimeathiriwa zaidi ni zile zinazopakana na mataifa ya eneo la IGAD, ambayo ni pamoja na Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini, na Djibouti. Serikali ya kitaifa na pia za Kaunti, washirika wa kimataifa na pia mashirika mbali mbali yamezindua mipango ya kuingilia kati ili kuwapunguzia mateso WaKenya milioni 3 ambao wanakabiliwa na baa hilo la njaa.