Margaret Kenyatta apongeza shirika la maskauti wa kike

Mama wa taifa Margaret Kenyatta amepongeza shirika la maskauti wa kike nchini kwa kusimama kidete kuhusiana na maswala ya heshima,uadilifu,huduma,uongozi na uzalendo tangu ubunifu wake.Alisema maadili yanayotokanna mafunzo ya shirika hilo la maskauti wa kike huwanufaisha maishani wanachama wa shirika hilo. Akiongea alipojiunga na wanachama wa shirika hilo kuadhimisha siku tafakari duniani inayosherekewa katika mataifa 150,mama wa taifa alipongeza shirika hilo kwa kuwapa wanawake msingi thabiti.Siku hiyo hushrekewa na zaidi ya maskauti milioni kumi wa kike duniani.