Marekani yawapongeza Uhuru na Ruto

Marekani imempongeza Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kufuatia kuapishwa kwao kuhudumu kwa kipindi cha pili uongozini.A�Katika risala ya pongezi msemaji wa wizara ya nchi za kigeni ya MarekaniA�Heather Nauert alisema Marekani inaendelea kujitolea kushirikiana na Kenya kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi sio tu hapa nchini bali pia eneo zima la afrika mashariki. Aliwahimiza wakenya kuungana na kumaliza migawanyiko iliyopo miongoni mwa jamii tofauti tofauti na makundi ya kisiasa ili kuwa na mwelekeo wa pamoja kusonga mbele. Nauert alielezea wasi wasi kuongezeka kwa hali tete ya kisiasa humu nchini ambayo mara kwa mara husababisha watu kupoteza maisha na mali kuharibiwaA�na akawaomba maafisa wa usalama kutumia nguvu kiasi kuwatawanya waandamanaji. Waziri wa uingereza anayehusika na maswala ya AfrikaA�Rory Stewart alitaja kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwa hatua itakayoiwezesha Kenya kusonga mbele baada ya kipindi kirefu cha uchaguzi. Stewart alikuwa hapa jijini Nairobi kwa hafla ya kuapishwa na akafanya mazungumzo na Rais Kenyatta baada ya hafla hiyo. Stewart ambaye aliwasilisha ujumbe wa pongezi kutoka kwa waziri mkuu wa Uingereza, na Ofisi ya mashauri ya nchi za kigeni na Jumuiya ya madola alisema katika taarifa na akamwalika Rais Kenyatta kwenye mkutano wa viongozi wa jumuiya ya madola jijini London mwaka ujao. Pia ilikuwa ni ziara yake ya kwanza rasmi hapa Kenya tangu kuteuliwa kama Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya kimataifa na mashauri ya nchi za kigeni na ofisi ya jumuiya ya madola hapo mwezi Juni.